Polisi wanachunguza kisa ambapo mwanamume mwenye umri wa miaka 30 alifariki baada ya kushuka kutoka kwa feri.
Mkuu wa polisi eneo la Likoni Willy Simba amesema mwanamume huyo alianguka na kuzirai baada ya kushuka kwa feri mwendo wa saa tano siku ya Jumatano mchana.
Kulingana na maafisa wa polisi wa huduma za kivuko hicho, mwanamume huyo ambaye alishuka kwenye feri ya MV Kwale alianguka na kufariki papo hapo.
Mwili wa mwanamume huyo uko katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya Makadara ukisubiri kufanyiwa uchunguzi.