Mwanamme mwenye umri wa miaka 23 alizirai na kuaga dunia jana katika kaunti ya Kwale, katika zoezi la kuwasajili makurutu wa kujiunga na huduma ya polisi.
Mwarika Mwalimua alianguka pindi tu baada ya kumaliza mbio za kilomita sita katika uwanja wa Baraza Park mjini Kwale.
Maelfu ya vijana wengine kote nchini walijitokeza ili kuteuliwa kujiunga na polisi. Hayo yakijiri, wakaazi wa Mombasa wanaitaka serikali kuzipa hospitali zote za kaunti hiyo vifaa vya matibabu.
Hii ni baada ya mvulana mwenye umri wa miaka minne kuaga dunia alipokuwa akifanyiwa oparesheni ya jicho katika hospitali kuu ya Pwani.
Jamaa zake wanasema madaktari waliondoa jicho lake moja alipopatikana na saratani na kuipelekea hali.