Mwanamume mmoja mwenye umri wa makamu amifikishwa mahakamani jijini Mombasa kwa mashtaka ya kumlawiti mtoto wa miaka mitatu.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Mshatakiwa, Cassian Safari Katana, alifikishwa mbele ya hakimu mkuu Teresia Matheka akidaiwa kulazimisha uume wake akikusudia kumlawiti mtoto huyo wa miaka 3 na pia kupapasa sehemu zake za siri akitumia uume wake. 

Mshukiwa anadaiwa kutekeleza unyama huo katika maeneo ya Kilindini jijini Mombasa mnamo Oktoba 27, 2016 katika shule ya chekechea ya High Leval.

Mshukiwa amekanusha mashtaka hayo nakuachiliwa kwa dhamana ya shilingi 300,000, kesi hio imepangwa kusikizwa tarehe November 30, 2016.