Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Mwanamume mmoja anayedaiwa kumlaghai mwenzake zaidi ya Sh9,000 atasalia rumande hadi mwaka ujao endapo atakosa baili ya Sh15,000 pesa taslimu.

Hii ni baada ya kuagizwa kutoa baili hiyo na mahakama moja ya Nakuru siku ya Alahamisi alipokana shtaka hilo la kumlaghai mwenzake fedha.

Upande wa mashtaka ulidai kwamba mshtakiwa, George Macharia, alimlaghai Henston Ng’ang’a Sh9,700 kati ya tarehe Oktoba 28 na Oktoba 29, 2015 kwa madai kwamba angemkodishia nyumba mjini Nakuru.

Mshtakiwa alikana shtaka hilo mbele ya Hakimu Mkuu wa Nakuru Doreen Mulekyo.

Macharia atarejea mahakamani tarehe Novemba 19 ambapo kesi dhidi yake itatajwa.

Kesi hiyo itasikizwa Januari 25, 2015.