Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Mwanamume mwenye umri wa miaka 30 anayedaiwa kuiba vipande vya mbao vyenye thamani ya Sh500,000 kutoka kampuni ya mbao ya Transafaric iliyoko Nakuru amefikishwa mbele ya mahakama ya Nakuru kujibu shtaka hilo.

Mshtakiwa John Baruthi anadaiwa kuiba vipande hivyo vya mbao vyenye uzani wa tani 15 kutoka kwa kampuni hiyo inayomilikiwa na Zakayo Waweru kwa ushirikiano na wengine ambao hawakuwa kortini kati ya tarehe Septemba 18 na tarehe Octoba 3,2015.

Hata hivyo, Okinda aliyefikishwa mbele ya Hakimu Joel Ng’eno siku ya Jumanne alikana mashtaka hayo na kusema kuwa hajahusika na wizi huo huku akitaka mahakama hiyo imwachilie huru.

Hakimu Ng’eno alimpa mshtakiwa nafasi ya kuelewana na mlalamishi nje ya mahakama akisema endapo wataafikia makubaliano, wanaweza kuondoa kesi hiyo kortini.

Pamoja na hayo, alimtoza Okinda thamana ya Sh200,000 pesa taslimu.

Kesi hiyo itasikizwa Novemba 13, 2015.