Jengo la mahakama ya Mombasa.Mshukiwa wa ubakaji afungwa maisha.[Picha/the-star.co.ke]
Mwanamume mwenye umri wa makamo anayedaiwa kumbaka mtoto mwenye umri wa miaka 11 amefungwa kifungo cha maisha katika mahakama ya Mombasa.
Charles Mwaniki Njeru , anadaiwa kutekeleza kisa hicho kati ya Novemba 8 na 11 mwaka wa 2016, katika mtaa wa Chaani eneo bunge la Changamwe.
Akitoa uamuzi huo hakimu Edgar Kagoni amesema kuwa ushahidi uliotolewa umeonyesha wazi mshukiwa alimbaka mtoto huyo.
Kagoni amesema hukumu hiyo itakuwa funzo kwa wengine wanaolenga kuwadhulumu watoto wadogo kimapenzi.
Kagoni amevitaja visa vya dhulma za kimapenzi dhidi ya watoto zimezidi kuongezeka nchini hasa ukanda wa Pwani.
“Visa vya unyanyasaji wa kimapenzi kwa watoto wadogo vimezidi kushuhudiwa mara kwa mara nchini, hivyo basi hukumu kali zinafaa kuwa funzo kwa wabakaji”,alisema Kagoni.
Mshukiwa yuko na siku 14 kukata rufaa.