Jengo la Mahakama ya Mombasa. [Photo/ the-star.co.ke]
Mwanamume mmoja amefikishwa mbele ya Mahakama ya Mombasa kujibu shtaka la wizi.Mwalimu Bakari anadaiwa kuiba shilingi elfu 10 pamoja na spika mbili za redio zenye thamani ya shilingi elfu nane katika eneo la Likoni mnamo Juni 6, mwaka huu.Bakari alikubali shtaka hilo mbele ya Hakimu Edgar Kagoni siku ya Jumatano.“Nakubali niliibia pesa hizo pamoja na spika hiyo. Naomba msamaha na nawaahidi kuwa sitorudia kosa hilo tena,” alisema Bakari.Hakimu Kagoni alimhukumu Bakari kwa kifungo cha miaka miwili gerezani.Akitoa uamuzi huo, Hakimu Kagoni alisema kuwa kifungo hicho kitakuwa funzo kwa wengine wanaoendeleza tabia ya wizi hasa katia eneo la Likoni.