Share news tips with us here at Hivisasa

Mwanamume mwenye umri wa makamo alifikishwa mbele ya mahakama moja mjini Eldoret  akishtakiwa kwa kosa la kuuza pombe haramu .

Michael Kamau alifikishwa mahakamani siku ya jumatatu kwa kosa la kuuza Zaidi ya lita 10 za changaa katika eneo la Langas.

Kamau alikubali mashtaka na akajitetea mbele ya hakimu mkuu mkaazi Pauline Mbulika kuwa yeye ndiye anayetegemewa na familia.

Mahakama iliamuru mshitakiwa alipe faini ya shilingi elfu kumi au ahudumu kifungo cha miezi sita gerezani.

Aidha, mwanamke mmoja alishtakiwa katika mahakama hiyo kwa kuwa mlevi chakari na kuwatupia wananchi maneno ya matusi.

Lydia muthoni alikubali makossa yake na kujitetea kwa kusema kuwa alikuwa na mawazo mengi ndio maana akaamua kunywa pombe.

Aliamuriwa kulipa faini ya shilingi 500 ama kifungo cha siku kumi na nne gerezani.