Mwanamume mwenye umri wa makamo amehukumiwa kifo baada ya kupatikana na kosa la kuwalawiti watoto watatu.

Share news tips with us here at Hivisasa

Mahakama ilielezwa kuwa Raphael Medadi alitekeleza kitendo hicho katika eneo la Manyatta, Likoni, mnamo February mwaka 2013.

Hakimu katika Mahakama ya Mombasa Daglous Ogoti, amesema ushahidi uliotolewa na watoto hao unaambatana, hivyo basi kuweka wazi kuwa mshukiwa alitekeleza kosa hilo.

“Ushahidi wa waathiriwa unaaambatana na kisheria ushahidi wa watoto unakubalika bila pingamizi,” alisema Ogoti.

Wakitoa ushahidi wao, watoto hao waliambia mahakama kuwa walipewa mabuyu, kisha kushikwa na usingizi wakiwa katika nyumba ya mshukiwa.

Aidha, waliambia mahakama kuwa walipoamka, walijipata bila nguo huku wakihisi uchungu kwenye sehemu nyeti.

Hakimu Ogoti alisema uchungzi wa madaktari pia unaonyesha kuwa watoto hao walilawitiwa.

Medadi alipewa siku 14 kukata rufaa.