Mwanamume mmoja amefungwa miaka 20 jela baada ya kupatikana na hatia ya ubakaji.
Nyanje Mwero, mwenye umri wa makamo, anadaiwa kumnajisi msichana wa miaka ya 15 mnamo Machi 27 katika maeneo ya Majengo Mapya gatuzi dogo la Likoni.
Akitoa uamuzi wake, Hakimu Martin Rabera alisema kulingana na ushahidi uliotolewa, ni wazi kuwa jamaa huyo alitekeleza kitendo hicho.
“Nimetilia maanani ushahidi uliotolewa na mtoto huyo pamoja na mashahidi wengine katika kesi hii. Sina budi kumfunga mshtakiwa miaka 20 jela kwa kosa hilo,” alisema Rabera.
Mwero alipewa siku 14 kukata rufaa.