Jengo la mahakama ya Mombasa. [Picha/ the-star.co.ke]
Mwanamume mmoja mwenye umri wa makamo amehukumiwa kifungo cha miaka 30 gerezani baada ya kupatikana na hatia ya ubakaji wa msichana mwenye umri wa miaka 13.Alphonce Mlando anadaiwa kumnajisi msichana huyo wa darasa la nne katika eneo la Mishomoroni eneo bunge la Kisauni mnamo Machi 10 na 11 mwaka huu.Kulingana na ushahidi uliotolewa mahakamani, mtoto huyo alibakwa akiwa ametoka shuleni nyakati za mchana.Akitoa uamuzi huo siku ya Jumatano, Hakimu Edger Kagoni alisema kuwa hukumu hiyo itakuwa funzo kwa wale wanaowabaka watoto wadogo.“Kifungo hiki kitakuwa onyo kwa wanaolenga kuvunja sharia kwa kuwabaka watoto wadogo hasa eneo hili la Mombasa,” alisema Kagoni.Hakimu huyo alisema ni jambo la kusikitisha kuwa visa vya kuwadhulumu kimapenzi watoto wa shule ambao hawajatimiza umri wa miaka 18 vimezidi kushudiwa kila mara katika maeneo mbali mbali.“Visa vya dhuluma za kimapenzi vimezidi mno hasa dhidi ya wanafunzi wa shule ambao hawajatimiza miaka 18, hatua ambayo ni ukiukaji wa haki za watoto,” alisema Kagoni.
Is there a newsworthy accident, incident or event happening in Mombasa County that you want Hivisasa to cover? Tell us what is happening by joining this group and have it published. http://bit.ly/2BipYa6