Jengo la Mahakama ya Mombasa.[Picha/ the-star.co.ke]

Share news tips with us here at Hivisasa

Kijana mwenye umri wa makamo amehukumiwa kifungo cha miaka 30 gerezani kwa kosa la kumbaka mtoto mwenye umri wa miaka 11.Upande wa mashtaka ulieleza mahakama kuwa Alex Mutiso Mumo alitekeleza kisa hicho katika eneo la Chaani mnamo Julai 27, 2017.Akitoa uamuzi huo siku ya Jumanne, Hakimu Edgar Kagoni wa Mahakama ya Mombasa alisema kuwa ushahidi uliotolewa unadhihirisha wazi kuwa Mumo alimbaka mtoto huyo.“Kulingana na ushahidi uliotolewa ni wazi kuwa mshukiwa ndiye aliyembaka mtoto huyu,” alisema Hakimu Kagoni.Kagoni alisema kuwa hukumu hiyo itakuwa kama funzo kwa wale ambao wanahusika katika tabia ya ubakaji wa watoto wadogo.“Hukumu hii itakuwa funzo kwa wengine wenye nia na njama ya kuwabaka watoto katika eneo hili la Mombasa,” alisema Kagoni.Aidha, ameongeza kuwa visa vya ubakaji vimezidi hasa kwa watoto wadogo katika maeneo mengi ya Pwani, na kuonya kuwa mahakama itawakabili wanaoendeleza visa hivyo.“Visa vya ubakaji vimezidi sana eneo la Pwani. Mahakama itawachukulia hatua kali wanaojihusisha na visa hivyo,” alisema Kagoni.