Mahakama ya Mombasa imemhukumu mwanamume mmoja kifungo cha miaka mitano gerezani kwa kosa la kumlawiti mvulana mwenye akili taahira.
Upande wa mashtaka ulielezea mahakama kuwa mshukiwa, Ibrahim Ramadhani, alitekeleza kitendo hicho katika eneo la Shelly Beach Likoni, tarehe 30 mwezi wa Octoba mwaka jana.
Akitoa hukuma yake siku ya Alhamisi, Hakimu Susan Shitubi alisema kuwa ushahidi wa mashahidi wanne unadhihirisha mshtakiwa alimlawiti mvulana huyo.