Mwanamume mmoja mwenye umri wa makamo amefungwa kifungo cha miaka mitatu gerezani kwa kosa la kupatikana na dawa za kulevya.
ADVERTISEMENT
Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!
Mshukiwa, Harison Opunde, alipatikana na vipakiti 11 za dawa aina ya heroine mnamo Machi 20, mwaka huu, katika eneo la Likoni.
Hakimu Mkuu Susan Shitub alitoa kifungo hicho Siku ya Jumatano baada ya Opunde kukubali kosa hilo.
Opunde alipewa siku 14 kukata rufaa kupinga uamuzi huo.