Mwanamume mmoja amehukumiwa kifungo cha miaka miwili gerezani baada ya kupatikana na hatia ya ulaghai.
Mshtakiwa, Ibrahim Yusuf, alipatikana na hatia ya kuwalaghai wananchi kwa kujifanya kuwa afisa wa polisi.
Mshtakiwa huyo pia alipatikana na hatia ya kuwaibia wakaazi katika eneo la Likoni, Kaunti ya Mombasa, kabla ya kukamatwa mwezi Agosti mwaka jana.
Katika shtaka lingine, mahakama iliagiza mshtakiwa huyo kulipa faini ya shilingi elfu 50 au kutumikia kifungo cha mwezi mmoja gerezani kwa kosa la kumuibia Rama Shaaban simu yenye thamani ya shilingi elfu 22.
Akitoa hukumu yake siku ya Jumatatu, Hakimu Teresia Matheka alisema kuna ushahidi wa kutosha kuhusu mashtaka hayo.
Hakimu Matheka aliagiza mshtakiwa huyo kukata rufaa chini ya siku 14 iwapo hajaridhishwa na hukumu aliyopewa.