Share news tips with us here at Hivisasa

Mzee mwenye umri wa miaka 50 alifikishwa mahakamani siku ya Jumanne kwa shtaka la kuiba kioo cha gari.

Upande wa mashtaka ulielezea mahakama kuwa mshukiwa, Said Rashid, anadaiwa kuiba kioo cha gari chenye thamani ya Sh10,000, mali ya Amani Rashid, katika eneo la uwanja wa Makadara, jijini Mombasa Mnamo Novemba 16, 2015.

Hakimu Diana Mochache alimhukumu Rashid kifungo cha miezi 15 gerezani, na kusema kuwa hukumu hiyo itakuwa funzo kwa wengine wanaojihusisha na wizi wa vioo vya magari nchini.