ADVERTISEMENT
Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!
Mwanamume mmoja amefikishwa mbele ya Mahakama ya Mombasa kwa kosa la kutoroka jela.
Upande wa mashtaka ulielezea mahakama siku ya Jumatano kuwa mshtakiwa, Paul Mutua, alitoroka jela tarehe 3 mwezi Mei.
Mahakama iliambiwa kuwa mshtakiwa huyo alitoroka maafisa wa polisi walipokuwa wakimpeleka katika Hospitali kuu ya Mkoa wa Pwani kubaini umri wake.
Hakimu Douglas Ogot alimhukumu kifungo cha mwaka mmoja gerezani.