Mwanamume mwenye umri wa miaka 28 amefikishwa kizimbani kwa kosa la kumpiga mamake.

Share news tips with us here at Hivisasa

Bakari Ali andaiwa kuzua fujo na kumshambulia mamake mnamo Januari 25, mwaka huu katika mtaa wa Kisumu Ndogo eneo bunge la Changamwe.

Bakari alikubali kosa hilo mbele ya Hakimu Edgar Kagoni siku ya Jumatatu katika Mahakama ya Mombasa.

Hata hivyo, Bakari alijitetea kwa kusema kuwa alikuwa mlevi wakati wa tukio hilo.

“Ni ukweli nilimpiga mamangu kwa sababu nilikuwa nimelewa,” alisema Bakari.

Hakimu Kagoni alimtoza Bakari faini ya shilingi elfu kumi ama kifungo cha siku saba jela.

“Kwa vile umekubali kosa lako, basi mahakama imekufunga siku saba gerezani au ulipe faini ya shilingi elfu kumi,” alisema Kagoni.