Mwanamme mmoja mwenye umri wa miaka 42 mjini Molo amejitia kitanzi baada ya mzozo wa kinyumbani.
Mwili wa Wilson Kibet Koskey ulipatikana ukining’inia kwenye mlango wa chumba chao cha kulala Jumanne huku akitoa sababu za kujitoa uhai kwenye barua yake ya kurasa tano aliyokuwa ameiandika pamoja na histori fupi ya maisha yake.
Kwenye ujumbe huo, mwendazake amesema maisha yake yamekuwa ya changamoto nyingi ikiwemo maswala ya ndoa pamoja na kupokonywa mali yake na marafiki wake wa karibu pamoja na mkewe.
Aidha Jamaa huyo alitaja maonevu na kutofanikiwa vema katika maisha kama sababu ambazo zimemfanya kukata tamaa na ndio akajitoa uhai.
Wingu la simanzi lilitanda katika ploti anayoishi mwendazake huku wanaomjua wakimtaja kama mtu mnyamavu na mwenye bidii.
“Alikuwa mtu muungwana sana na tuliposikia amejitoa uhai tumeshangaa sana, hatukudhani anaweza kufanya hivo, ni huzuni sana,” alisema mmoja wa jirani wake.