Mwanamume mwenye umri wa makamo amewaacha wakaazi vinywa wazi katika Mahakama ya Mombasa baada ya kukubali shtaka la ubakaji.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Mshukiwa huyo, Kennedy Baraza, alimnajisi mtoto wa umri wa miaka 13 kati ya tarehe Juni 29 na Julai 7, mwaka huu, katika eneo la Kiwarera huko Likoni.

Baraza alikubali kutekeleza kisa hicho mbele ya Hakimu Lilian Lewa siku ya Jumatatu.

“Ni kweli nilifanya mapenzi na mtoto huyu. Tumekuwa na uhusiano wa kimapenzi kwa muda mrefu,” alisema Baraza.

Mahakama itatoa uamuzi wa hukumu ya kesi hiyo tarehe Julai 19, mwaka huu.