Mwanamume mmoja amefikishwa mbele ya Mahakama ya Mombasa kujibu shtaka la wizi.

Share news tips with us here at Hivisasa

Mshtakiwa huyo, Josephat Kitumbu, anadaiwa kuiba simu mbili zenye thamani ya zaidi ya shilingi elfu tisa.

Upande wa mashtaka ulielezea mahakama kuwa mshtakiwa huyo anadiawa kutekeleza kitendo hicho mnamo tarehe 24 mwezi Machi, katika eneo la Changamwe, Kaunti ya Mombasa.

Bwana Kitumbu alikubali shtaka hilo mbele ya Hakimu Julias Nang'ea, siku ya Jumatano.

Hakimu Nang'ea alisema kuwa atatoa hukumu yake baadaye.