Mwanamume mmoja ameishtaki kampuni ya mabasi ya Mbukinya, baada ya kudaiwa kugongwa na basi moja la kampuni hiyo.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Kwa mujibu wa kesi aliyowasilisha kwenye Mahakama kuu ya Kisumu siku ya Jumatatu, mlalamishi, Oliver Owino, alisema kuwa aligongwa na basi moja la kampuni ya mabasi ya Mbukinya, mnamo tarehe saba mwezi Machi mwaka jana, katika eneo la Rabuor, kwenye barabara kuu ya Kisumu-Nairobi.

Owino alisema kuwa kando na kupata majeraha mbali mbali ya mwili, alipoteza shilingi alfu 126, alizokua akienda kutumia kununua bidhaa za hoteli wakati alipogongwa na basi hilo.

Aliitaka kampuni hiyo imlipe pesa hizo, pamoja na pesa zote alizotumia kwenye matibabu katika Hospitali ya Mafunzo na Rufaa ya Jaramogi Oginga Odinga, al maarufu Russia jijini Kisumu.

Hakimu mkaazi wa Mahakama kuu ya Kisumu Thomas Ogutu, aliahirisha kesi hiyo hadi tarehe 17 mwezi Mei mwaka huu.