Mtoto wa umri wa miaka saba anaendelea kupokea matibabu katika hospitali ya Nairobi Women tawi la Nakuru, baada ya kunajisiwa katika kituo cha kibiashara cha Maili Sita, Bahati.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Aidha, mtoto huyo ambaye alinajisiwa Jumanne jioni, alikuwa amepelekwa katika hospitali ya kaunti ndogo ya Bahati.

Inasemekana mtoto huyo alitendewa unyama huo na mshukiwa ambaye ni jirani yao katika kituo cha kibiashara cha Maili Sita, wakati mamake alikuwa ameenda kibarua.

Kulingana na mhudumu msimamizi katika hospitali hiyo Angela Gwaro, mtoto huyo wa darasa la pili alipata majeraha makali kutokana na kitendo hicho cha unyama japo alidokeza kuwa hali yake ya afya imeimarika.

Dkt Gwaro alidokeza kuwa visa vya unajisi vinavyoripotiwa katika hospitali hiyo vinaongezeka kila kuchao.

“Kuna haja ya kuhamasisha wananchi jinsi ya kujiepusha na maswala kama ya ubakaji, na mengine potovu katika jamii,” alisema Dkt Gwaro.

OCPD wa Nakuru Kaskazini Duncan Nguthu alithibitisha kukamatwa kwa mshukiwa huyo aliyetambulika kwa jina moja kama Joel, akisema atafikishwa mahakamani uchunguzi utakapokamilika.