Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Mahakama kuu ya Mombasa imemuachilia huru mwanamume anayedaiwa kumuua mkewe na kisha kumchoma.

Risley Levers Kavu anadaiwa kumuua mkewe Natalie Kellsall, mnamo Septemba 17, 2013 katika eneo la Utange huko Kisauni.

Akitoa uamuzi wake siku ya Alhamisi, Jaji Martin Muya alisema kuwa upande wa mashtaka umeshindwa kuweka wazi aliyehusika katika mauaji hayo.

Aliongeza kuwa maafisa wa upelelezi walishindwa kufanya uchunguzi wa kutosha kuhusiana na kifo hicho, ili kuweka wazi washukiwa wakuu.

Aidha, aliongeza kuwa mashahidi wote wa kesi hiyo waliambia mahakama kuwa hawakumuona mshukiwa akimuua wala kumchoma mwendazake.