Jengo la Mahakama ya Mombasa. [Picha/ the-star.co.ke]
Mshukiwa anayedaiwa kutekeleza mauaji ya raia wawili wa Uswizi atazuiliwa korokoroni kwa muda wa siku 21 zaidi kabla ya kufunguliwa mashtaka.
Haya yanajiri baada ya majaji wanaosikiza kesi za mauaji kuenda likizo.Geoffrey Mwaki anadaiwa kuhusika katika mauaji ya Paul Werner Borner na Marianne Borner mnamo Agosti 21, 2017 katika msitu wa Nguu Tatu eneo la Kiembeni, Kisauni.Mwaniki alipaswa kufunguliwa mashtaka siku ya Jumanne lakini kesi hiyo ikaairishwa baada ya majaji kukosa kufika mahakamani.Hakimu George Kiage ambaye pia ni naibu msajili katika Mahakama ya Mombasa, ameagiza kesi hiyo kutajwa Septemba 26, 2017 mbele ya Jaji Asenath Ongeri.Kiage vile vile aliagiza kijana anayedaiwa kumuua mchumba wake kuzuiliwa kwa muda wa siku 21.Samuel Malava anadaiwa kumuua mchumba wake Salome Kathami mnamo Agosti 30, 2017 katika eneo la Shauri Yako eneo bunge la Kisauni.Kiage aliagiza Malava kuzuiliwa katika gereza la Shimo la Tewa hadi pale majaji wa mahakama kuu watakaporudi kutoka likizo.Aidha, Kiage aliagiza mshukiwa huyo kuchunguzwa akili kabla ya kufunguliwa mashtaka.“Utafanyiwa uchunguzi wa akili kabla ya kufunguliwa mashtaka mbele ya Jaji Asenath Ongeri,” alisema Kiage.Malava atatafutiwa wakili na mahakama kwa kuwa hana uwezo wa kulipa wakili wake binafsi.Kesi hiyo itatajwa Septemba 26, 2017.