Polisi mjini Mombasa wanafanya uchunguzi wa mwanamume mmoja aliyepatikana amefariki katika hoteli ya Summerlink mjini Mombasa siku ya Jumatatu alasiri.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Akidhibitisha kisa hicho naibu mkuu wa polisi katika kaunti ya Mombasa Patrick Njoroge amesema kuwa idara ya usalama kwa sasa haijamtia mtu yeyote mbaroni kwa kuhusika na kifo hicho huku akisema kuwa upelelezi na uchunguzi zaidi bado unafanywa.

Hata hivyo, imebainika kuwa mwanaume huyo alikuwa amelala hotelini humo na mpenzi wake wa kike ambaye ametoweka hadi sasa, huku dawa za kuongeza nguvu za kufanya mapenzi na mipira za kondomu zikipatikana katika chumba chao.

kwa sasa maafisa wa polisi wameanza msako dhidi ya mpenzi wake aliyetoweka na kusema kuwa bado hawajamtambua mwananume huyo kwa kuwa hakuna stakabadhi zozote za kujitambulisha zilipatikana chumbani.