Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Mzee wa miaka 60 amefikishwa mahakamani kwa shtaka la kutuma ujumbe wenye matusi kupitia simu ya rununu.

Mahakama ilielezwa siku ya Jumatatu kuwa mnamo Novemba 5,2015 Abdulhakimu Mohamed anadaiwa kumtumia Mohamed Ali Swaleh ujumbe uliokuwa na dhamira ya kuzua chuki kati yao.

Mohamed alikanusha madai hayo mbele ya hakimu mkuu wa Mombasa Susan Shitub na kutozwa dhamana ya Sh50,000 ama Sh20,000 pesa taslimu.

Kesi hiyo itatajwa Novemba 30, 2015.