Share news tips with us here at Hivisasa

Mwanamume mmoja ameshtakiwa katika Mahakama ya Mombasa kwa madai ya ubakaji.

Mshukiwa, Stephen Otieno, anadaiwa kumbaka msichana wa miaka 18 mwenye akili tahira.

Upande wa mashtaka ulielezea mahakama siku ya Jumanne kuwa mshukiwa alitenda kitendo hicho mwisho wa mwaka jana katika eneo la Changamwe, Kaunti ya Mombasa.

Mshtakiwa huyo alikana shtaka hilo Mbele ya Hakimu Susan Shitubi na kutaka kuachiliwa kwa dhamana.

Kesi hiyo itatajwa tarehe Aprili 22, 2016.