ADVERTISEMENT
Share news tips with us here at Hivisasa
Mwanamume mmoja ameshtakiwa katika Mahakama ya Mombasa kwa madai ya wizi.
Mshtakiwa huyo, John Ogweno, anadaiwa kuiba mali yenye thamani ya zaidi ya shilingi laki mbili katika eneo la Treasury Square, jijini Mombasa, mnamo tarehe tano mwezi wa Aprili.
Hatahivyo, mshukiwa huyo alikana shtaka hilo linalomkabili mbele ya Hakimu Irene Ruguru siku ya Jumatatu.
Hakimu Ruguru aliagiza kesi hiyo kusikizwa tarehe 7 mwezi wa Juni.