Mwanamume mmoja ameshtakiwa katika Mahakama ya Mombasa kwa kuendesha biashara bila leseni.
Mshtakiwa, Wilson Wanga, anadaiwa kuendesha biashara hiyo ya kuuza majani chai katika eneo la Mwembe Tayari, Kaunti ya Mombasa, bila kibali kutoka kwa idara husika.
Mahakama iliambiwa siku ya Jumatano kuwa mshukiwa anadaiwa kukamatwa tarehe 29 mwezi Aprili, akiwa na gunia tatu za majani chai yenye thamani ya shilingi elfu 90.
Bwana wanga alikubali shtaka hilo mbele ya Hakimu Douglas Ogot.
Hakimu Ogot aliaagiza mshtakiwa huto kuregeshwe mahakamani siku ya Ijumaa kusomewa hukumu yake.