Mwanamume mmoja amefikishwa katika Mahakama ya Mombasa kujibu shtala la wizi.
Mhtakiwa, Johnstone Mutua, anadaiwa kuiba tuktuk yenye thamani ya shilingi laki mbili mjini Mombasa.
Upande wa mashtaka uliambia mahakama kuwa Mutua anadaiwa kutekeleza wizi huo tarehe 14 mwezi Machi, mwaka huu.
Mshukiwa huyo alikana mashtaka hayo siku ya Jumatatu mbele ya Hakimu Diana Mochache.
Hakimu Mochache aliagiza mshtakiwa huyo kuachiliwa kwa dhmana ya shilingi laki tatu.
Kesi hiyo itasikizwa tarehe 14 mwezi Juni.