Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Mwanamume mmoja amekana madai ya kutishia kumuua shahidi wa kesi inayomkabili katika Mahakama ya Mombasa.

Mshtakiwa huyo, Mwanaharusi Mwinyi, anadaiwa kutishia kumua Christine Awino, mnamo tarehe 15 mwezi Machi, alipokuwa akitoa ushahidi dhidi yake mahakamani.

Upande wa mashtaka umetaka mahakama kutomwachilia mshtakiwa huyo kwa dhamana kwa madai kuwa huenda akasambaratisha kesi yake ya awali.

Akitoa uamuzi wake siku ya Jumatano, Hakimu Julias Nang’ea, aliagizia mshukiwa kuendelea kuzuiliwa hadi tarehe 26 mwezi Mei, kesi hiyo itakaposikizwa.