Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Mwanamume mmoja ameshtakiwa katika Mahakama ya Mombasa kwa madai ya ubakaji.

Mshtakiwa huyo, Charles Maina, anadaiwa kumbaka msichana mwenye umri wa miaka tano mnamo tarehe 17 mwezi Aprili.

Bwana Maina alikana shtaka hilo siku ya Ijumaa mbele ya Hakimu Geoffrey Kimanga.

Hakimu Kimanga aliagiza mshtakiwa huyo kuachiliwa kwa dhamana ya shilingi laki tatu.

Kesi hiyo itasikizwa tarehe 23 mwezi Juni.