Mwanamume mmoja ameshtakiwa katika Mahakama ya Mombasa kwa madai ya ulanguzi wa binadamu.
Upande wa mashtaka ulielezea Mahakama kuwa mshukiwa, Robert Meti, alikamatwa siku ya Alhamisi katika eneo la feri kwa madai ya kusafirisha raia sita wa Ethiopia kuelekea Lunga Lunga.
Mshukiwa huyo alikana shtaka hilo mbele ya Hakimu Diana Mochache siku ya Ijumaa.
Raia hao wa Ethiopia hawakusomewa mashtaka yao kwa sababu ya kukosa mkalimani.
Hatahivyo,Hakimu Mochache aliagiza wasita hao kuendelea kuzuiliwa hadi siku ya Jumatatu watakaposhtakiwa.
Kesi hiyo itasikizwa tarehe 16 mwezi Juni.