Share news tips with us here at Hivisasa

Mwanamume mmoja amefikishwa katika Mahakama ya Mombasa kujibu shtaka la wizi wa mifugo.

Mshukiwa, Bonface Musyoka, anadaiwa kuiba ng’ombe wawili wenye thamani ya zaidi ya shilingi elfu 60.

Upande wa mashtaka ulieleza mahakama siku ya Jumatatu kuwa mshtakiwa anadaiwa kutekeleza wizi huo tarehe 24 mwezi Machi, katika eneo la Mazeras.

Mshtakiwa huyo alikana shtaka hilo mbele ya Hakimu Irene Ruguru.

Hakimu Ruguru aliagizia Musyoka kuachiliwa kwa dhamana ya shilingi laki mbili.

Kesi hiyo itasikizwa tarehe 6 mwezi wa Juni.