Share news tips with us here at Hivisasa

Mtu mmoja amefariki usiku wa kuamkia Alhamisi huku mali ya dhamani kubwa ikiteketea kufuatia mkasa wa moto katika mtaa mmoja wa makaazi mjini Naivasha.

Mwanamume huyo Samuel Njoroge mwenye umri wa miaka 42 alichomeka kiasi cha kutotambulika wakati wa kisa hicho katika mtaa wa County Council eneo hilo.

Mkazi mmoja Joseph Gachie amesema kuwa mwendazake alionekana akiwa mlevi na kuasha mshumaa ambao unakisiwa kuwa ulisababisha moto huo.

Gachie ameongeza kuwa nyumba yake pia iliyokuwa imetengenezwa kwa mbao ilichomeka kabla ya majirani waliouona moto huo kufika na kuuzima.

“Huwa anawasha mshumaa katika nyumba yake na ni nyumba iliyojengwa kwa mbao, na tunafikiria ndio iliyosababisha kuchomeka kwa nyumba yake,” alisema Gachie.

Polisi baadaye walifika eneo hilo na kuuchukua mwili huo na kuupeleka katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali kuu ya wilaya ya Naivasha.