Mwanamume mwenye umri wa makamo amefikishwa mahakamani kujibu shtaka la kuendeleza uvuvi bila kibali.
Upande wa mashtaka uliambia mahakama siku ya Jumatatu kuwa mshtakiwa, Hassan Juma, anadaiwa kupatikana akiendeleza uvuvi huo katika eneo la lango nambari 21 katika Bandari ya Mombasa, eneo lilisilofaa kutumika kwa uvuvi, mnamo Machi 11, 2016.
Juma alikubali makosa hayo Mbele ya Hakimu Susan Shitub na kutozwa faini ya shilingi 5,000 ama kutumikia kifungo cha miezi miwili gerezani.