Share news tips with us here at Hivisasa

Mwanamume mmoja ameshtakiwa katika Mahakama ya Mombasa kwa madai ya ubakaji.

Mshtakiwa huyo, Evans Ochola, anadaiwa kutekeleza kitendo hicho tarehe 17 mwezi Aprili katika eneo la Likoni.

Mshukiwa huyo alikana shtaka hilo mbele ya Hakimu Diana Mochache siku ya Jumnne.

Hakimu Mochache aliagiza kuachiliwa kwa mshukiwa huyo kwa dhamana ya shilingi laki mbili.

Kesi hiyo itasikizwa tarehe 15 mwezi Juni.