Mwanamume mmoja amefikishwa katika Mahakama ya Mombasa kujibu shtaka la ulaghai.
Mshukiwa, Erick Wabwire, anadaiwa kumlaghai mlalamishi Peter Mukiri zaidi ya shilingi laki nane, mwezi Machi kati ya tarehe 23 na 29 kwa kumdanganya kuwa atamuzia gari.
Mshukiwa huyo alikana madai hayo mbele ya Hakimu Diana Mochache siku ya Jumatatu.
Upande wa mashtaka uliwasilisha ombi la kumtaka mshukiwa asiwachiliwe kwa dhamana hadi atakapotoa stakabadhi zake za kujitambulisha.
Hakimu Mochache aliagiza mshukiwa huyo aendelee kuzuiliwa hadi siku ya Jumanne mahakama itakapotoa uamizi wa iwapo atawachiliwa kwa dhamana au la.