Jengo la Mahakama ya Mombasa. [Picha/ the-star.co.ke]
Mwanamume aliyejifanya kuwa afisa wa upelelezi kutoka kitengo cha kukabiliana na ufisadi ameachiliwa kwa dhamana.
Wesley Kipkemboi Kiptanui anadaiwa kujiwasilisha kwa Micheal Kingi, nduguye Gavana wa Kilifi Amason Kingi, akidai kumsaidia gavana huyo kukabiliana na kashfa za ufisadi zinazomkumba.Maafisa wa usalama walimnasa mshukiwa huyo mnamo Juni 2 mwaka huu, baada ya Michael kuripoti kisa hicho.Hata hivyo, Kiptanui alikanusha mashtaka hayo siku ya Jumatatu mbele ya Hakimu katika Mahakama ya Mombasa Francis Kyambia.Alisema kuwa yeye na Micheal ni marafiki wa karibu na alikuwa ameenda kumtembelea.“Micheal Kingi amekua rafiki yangu kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa. Nilikuwa nimeeda kwake kumjulia hali,” alisema Kiptanui.Hakimu Kyambia alimuachilia kwa dhamana ya shilingi laki tano ama shilingi laki mbili pesa taslimu.