Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Mwanamume mmoja ameshtakiwa katika Mahakama ya Mombasa kwa madai ya wizi.

Mshtakiwa, Victor Ogola, anadaiwa kuiba mita za umeme aina ya 'post-pay' zenye thamani ya shilingi laki 80, mali ya kampuni ya Kenya Power mnamo tarehe 4, mwezi Mei.

Mshukiwa huyo alikana madai hayo mbele ya Hakimu Douglas Ogot siku ya Jumatano.

Hakimu Ogot aliagiza Bwana Ogola kuachiliwa kwa dhamana ya shilingi elfu 40, au shilingi elfu 25 pesa taslimu.

Kesi hiyo itasikizwa tarehe 16 mwezi Mei.