Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Kesi ya mwanamume anayedaiwa kutengeneza hati miliki bandia ya kipande cha ardhi chenye thamani ya mamilioni ya pesa, imefanyiwa marekebisho katika Mahakama ya Mombasa.

Haya yanajiri baada ya upande wa mashtaka kuwasilisha ombi la kutaka marekebisho hayo kufanywa.

Mshtakiwa, John Ngure, anadaiwa kutengeneza hati bandia ya kumiliki ploti ya hekari mbili katika eneo la Nyali, mjini Mombasa, yenye thamani ya shilingi milioni 350.

Mshukiwa huyo anadaiwa kutengeneza hati miliki hiyo kati ya mwaka 1996 na 2014.

Bwana Ngure alikana shtaka hilo mbele ya Hakimu Julias Nang’ea siku ya Jumatano.

Hakimu Nang’ea aliagiza mshtakiwa huyo kuachiliwa kwa dhamana ya shilingi milioni moja.

Kesi hiyo itasikizwa tarehe 6 mwezi Julai.