Mwanamume mwenye umri wa makamo amefikishwa mahakamani kujibu shtaka la kutumia lugha ya matusi.

Share news tips with us here at Hivisasa

Mwendesha mashtaka Erick Masila aliambia mahakama kuwa mshtakiwa, Juma Kibubu, anadaiwa kutumia lugha ya matusi na kumuita mlalamishi Bihasha Ahmed mchawi, mnamo Mei 11, 2016, katika eneo la Shika Adabu huko Likoni.

Kibubu pia alikabiliwa na shtaka na pili la kutishia kumua mlalamishi huyo.

Hata hivyo, mshtakiwa huyo alikanusha mashtaka hayo siku ya Jumanne mbele ya Hakimu mkuu Teressia Matheka.

Mtuhumiwa aliachiliwa kwa dhamana ya shilingi 20,000.

Kesi hiyo itasikizwa Juni 20, 2016.