Mwanamume mmoja amefikishwa katika Mahakama ya Mombasa kujibu shtaka la ulaghai.
Upande wa mashtaka ulielezea mahakama siku ya Jumanne kuwa mshtakiwa huyo, Said Shekh, anadaiwa kujipatia zaidi ya shilingi elfu 80 kwa njia ya ulaghai.
Bwana Shekh anadaiwa kutekeleza kosa hilo tarehe 23 mwezi Februari katika eneo la Mwembe Tayari, Kaunti ya Mombasa.
Mshtakiwa huyo alikana madai hayo mbele ya Hakimu Daniel Ogoti.
Hakimu Ogoti aliagiza Bwana Shekh kuachiliwa kwa dhamana ya shilingi elfu 50.