Wingu la huzuni lilitanda katika kijiji cha Kathaana kaunti ya Machakos baada ya mwanaume mmoja kujitia kitanzi kwa sababu ya vita vya kinyumbani.

Share news tips with us here at Hivisasa

Mwili wa John Muthoka ulipatikana umeningi'a chumbani mwake huku akiwa ameacha barua iliyokuwa ikisema kuwa, "inaonekana hakuna anayeona dhamani yangu duniani heri niondoke niache kuwa mzigo kwenu".

Inadaiwa kuwa Muthoka alikuwa amegombana na mkewe siku iliyopita kuhusu pale pesa zingetoka za kumpeleka mtoto wao chuo kikuu ambaye alikuwa amepita vyema katika mtihani wa kidato cha nne.

Kulingana na mamake Muthoka, Sarah Kasiva, marehemu walizozana na mkewe ambapo mkewe kwa madai ya kuvuja mali.

Inasemekana kuwa wawili hao walikuwa wamekopa pesa za kumpeleka mwanao shuleni lakini marehemu akazitumia vibaya.

Inadaiwa kuwa mabishano yalipozidi mwanamke huyo alifunga virago na kurudi kwao huku akiacha amemwambia mumewe kuwa yeye ni mume bwege na kuwa anajutia kuolewa naye.

"Nilitoka nje jioni na kumpata kijana wangu na mkewe wakigombana kuhusu hatima ya kijana wao ambaye alikuwa amepasi mtihani wake wa kiadato cha nne,” asema Kasiva.

Kasiva anaendelea kuwa wawili hao hawakusikizana jinsi watapata pesa za kumfundisha mtoto wao hapo ndipo mkewe Muthoka aliamua kurundi kwao.

“Kutoka hapo Muthoka alijifungia chumbani chake cha kulala na asubuhi nilipomwita hakuitika,” akasema Kasiva.

Kwa sasa mwili wake umepelekwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti cha kangundo huku ukisubiri kuzikwa.