Jengo la Mahakama ya Mombasa. Picha: Haramo Ali/ hivisasa.com

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Mwanamume mmoja mwenye umri wa makamo amefikishwa katika Mahakama ya Mombasa kwa madai ya kueneza jumbe za uchochezi na chuki.

Hamisi Mohamed Fadhili anadaiwa kupatikana na nakala zenye maandishi ya kueneza chuki katika eneo la Kwale, mnamo Februari 16, mwaka huu.Nakala hizo zilikuwa zimeandikwa "Pwani Si Kenya", pamoja na kutishia jamii za Wapemba na Wamakonde na kuzitaka zirudi kwao.Hata hivyo, Fadhili alikanusha madai hayo mbele ya Hakimu Lilian Lewa.Hakimu Lewa alimuachilia Fadhili kwa dhamana ya shilingi laki mbili au shilingi laki moja pesa taslimu.Kesi hiyo itatajwa tena Machi 7.