Msanii wa Bongo Flava, Sam wa Ukweli amefariki.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Msanii huyo aliyetambulika kwa wimbo "Hata kwetu wapo" aliaga dunia asubuhi ya kuamkia Alhamisi, baada ya kuugua kwa muda mfupi.

Kwa mujibu wa taarifa za awali mwanamuziki huyo alianza kuugua akiwa studio na baadaye kukimbizwa katika hospitali ya Palestina kule Sinza Kinondoni, jijini Dar es Salaam.

Ripoti zasema  kwaajili ya matibabu lakini muda mchache alifariki dunia.

Akiongea na Millardayo usiku huo 

Prodyusa Steve Joniso ambaye alikuwa na marehumu mara ya mwisho alisema Sam alikuwa akilalamika kuumwa tumbo. Alizidiwa na kukosa nguvu kabisa hali ambayo na kumsababisha hata ashindwe kwenda chooni mwenyewe.

“Ikabidi tumpeleke chooni huwezi amini chooni tulimtenga hawezi kukaa kwenyewe, sisi tukaona hii sio kawaida, tukamwambia Sam ngoja tutoe taarifa kwa ndugu zako, yeye anakataa msiwataarifu, hiyo inaenda saa moja usiku, mida ya saa mbili usiku tukaamua kuwapigia simu ndugu zake tukawataarifu mbwana Sam yupo kwenye hali hii lakini amesema tusiwaambie kama mnaona vipi njooeni. Lakini baada muda mchache tukapigiwa simu na yule ndugu yake. Nimeongea na mke wake lakini amesema hana nauli kesho atakuja hapo kumuona, hata mimi nitakuja muda huo huo,” Steve alikiambia kituo moja Tanzania.

“Tumekaa mpaka saa nne usiku hali yake ikawa mbaya zaidi, akaomba akupumzike. Sisi tukamwambia tukupe dawa yeye akaomba apumzike ila kwa kunisaidia ili nisiwasumbue naomba nifunge pempasi, sisi kama vijana wa kiume tukamchukua tukamfunga pempasi, sisi tukarudi studio kuendelea na kazi,” aliongeza.

“Tumekaa dakika tano tu tukagongea kwamba Sam anawaita, kwenda kumuuliza vipi - Sam akasema siwezi kupumua vizuri, nasikia kama nashindwa kupumua. Sisi kwa upande wetu tukaona hii imekaa vibaya, tulichokifanya ni kumpeleka hospitali, tukampeleka mahabara ndogo pale Mabibo. Pale wakatuambia huyu jamaa anaumwa sana mpelekeni Palestina."

"Tumefika Palestina tumefanya process zote baadaye tukaambiwa tumpeleke kwenye emergency, wakawa wanamuekea vifaa vya kupumulia baadaye kama dakika 10 tukaitwa bwana nani anahusika? Nikasema mimi nahusika; wakaniambia njoo tukupe majibu, wakaniambia nijikaze huyu ndugu yako hatuko naye tena, sikuamini kwa sababu tulikuwa naye muda mchache uliopita na jana yake tulishinda naye,” alisema prodyusa huyo.