Mwanasiasa Ogeto Swanya  kutoka eneo bunge la Kitutu Masaba ameapa kuendelea kuwasaidia mayatima wa eneo bunge hilo kupata elimu.

Share news tips with us here at Hivisasa

Akiongea Ijumaa katika  hafla  ya mazishi ya mama  Mary Simeon kijiji cha Riamisiani wadi ya Gesima Ogeto alisema anataka kuinua kiwango cha masomo katika eneo bunge hilo.

  “Tunataka kila mmoja wetu aweze kuendeleza maisha yake bila matatizo. Kuwasaidia watoto wapate elimu ni njia moja ya kufanya maisha yao yawe bora,” akasema Ogeto.

Aidha, aliwaomba wakazi wote kushirikiana  ili kuinua viwango vya masomo  kwa kuwa ndio itasaidia kupata viongozi wa kesho.

Ogeto alisema kuwa atatembelea shule zote katika eneo hilo huku akiwatabua watoto mayatima.

Kwa upande mwingine aliwaomba viongozi waliomamlakani kwa sasa kuwasaidia wananchi ili kuinua viwango vya maendeleoo katika eneo bunge la Kitutu Masaba.

Alimwomba mwakilishi wa wadi ya Gesima Kennedy Nyameino  kukarabati baadhi ya barabara ambazo zimeharibika katika wadi ya Gesima ili kuwasaidia wakulima na wafanyibiashara.

 Ogeto pia alidokeza kuwa ameongea na Nyameino kuhusu ukarabati wa barabara ya Matunwa –Kiamitengi  na ile ya  Gesima – Esani- Magombo.