Mwaniaji wa kiti cha ugavana Kaunti ya Tana River Dadho Godana akiwahutubia wanahabari hapo awali. Picha/ kenya-today.com

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Mwanasiasa Dadho Godana ameikosoa serikali ya Jubilee kwa madai ya kushindwa kuinua wakaazi wa Pwani kiuchumi.Godana, ambaye ametangaza azma ya kuwania kiti cha ugavana Kaunti ya Tana River, alidai kuwa serikali imelibagua eneo la Pwani, na kuwataka wakaazi kujitenga na serikali hiyo.Akizungumza siku ya Jumanne katika eneo la Galole, Godana aliwahimiza wakaazi wa Pwani kuunga mkono upande wa upinzani, na kuongeza kuwa muungano wa NASA utapigania haki zao.Kiongozi huyo aliwasuta wanasiasa waliohamia upande wa serikali, na kudai kuwa walichukua hatua hiyo ili kujinufaisha binafsi.Aidha, amewataka magavana wa Pwani kusalia katika upinzani ili kupata nafasi ya kupigania haki za wakaazi.Godana alisema kuwa hatua hiyo itawawezesha Wapwani kupata ardhi na kunufaika moja kwa moja na raslimali za mashinani.Mbunge huyo wa zamani aliwashauri wakaazi kushirikiana na viongozi ili waweze kuvuna matunda ya ugatuzi.