Mfumo wa sasa wa elimu wa 8-4-4 una umuhimu na haufai kubadilishwa kama inavyopendekezwa na baadhi ya asasi, kulingana na mwanasiasa Dkt Stanley Karanja kutoka sub kaunti ya Nakuru mashariki.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Katika mahojiano ya kipekee, Karanja amedai kuwa huenda kuna watu wenye njama fiche katika swala hilo la kubadilisha elimu humu nchini. 

Karanja, ambaye pia ananuia kuwania kiti cha eneo bunge la Nakuru Mjini mashariki anasema kuwa mfumo wa sasa wa elimu wa 8-4-4 unamwezesha mwanafunzi kufahamu mengi. 

"Mimi mwenyewe nilipitia mfumo wa 8-4-4 na sijaona kama una changamoto," alisema Karanja. 

Wakati huo huo, amewataka wale wote wanaounga mkono mabadiliko ya mfumo huo kutafakari tena Kwa mara ya pili.

Isitoshe, amedai kuwa huenda kuna watu wanaonuia kunufaika kibiashara kuhusiana na swala la kubadilishwa mfumo wa 8-4-4. 

 Picha: Mwanasiasa wa Nakuru Dkt Stanley Karanja. Amepinga vikali swala la kubadilishwa mfumo wa 8-4-4, pendekezo ambao linaangaliwa kwa undani.